Friday 17 April 2015

Jinsi Ya Kubana Nywele Ndefu Za Asili

Mtindo huu wa kubana nywele ndefu za asili ni mtindo rahisi ambao unaweza bana mwenyewe nyumbani.

MAHITAJI
1.Chanuo
2.Mafuta
3.Chupio
4.Uzi

Hatua ya mwanzo chana nywele zako kwenda juu halafu funga uzi katikati ya nywele au ambapo unapendelea wewe.





 Baada yakuzifunga uzi nywele zako sasa ili kupata muonekano mzuri, chukua zile nywele za juu zinazo ning'inia alafu zifunge kijibutu hivi au ziokote kwakuzi kusanya pamoja.





Baada ya hapo chukua chupio alafu bana hapo kwenye kibutu, waweza tumia hizi chupio kubana nyuma kama nywele zinapepea na hazikubanika vizuri.


Kama ni mtoko sasa uko fresh kwakutoka.

5 comments: