Monday 27 April 2015

Afro

Huu ni mtindo wa kuchana nywele bila kusuka, nywele za saizi ya kati na ndefu hufaa zaidi. Katika mtindo huu nywele huchanwa kuelekea juu utosini na kutengeneza kitu mithili ya mwamvuli wa nywele.






Pia mtindo huu wa afro ni rahisi kutengeneza na hauhitaji gharama kubwa. Mtindo huu unafaa kutengenezwa kwaajili ya sherehe au mtoko wa jioni.

Rasta Za Asili:

Rasta za asili ni nywele za asili ambazo husokotwa badadala ya kusukwa. Mtindo huu huwa unahitaji nywele kukaa kwa muda mrefuu sana na unahitaji usafi wa hali ya juu, vingineyyo nywele zitatoa harufu

  


Mtindo huu wa rasta za asili kwa sasa hupendwa hutumiwa na jinsia zote mbili na nitofauti na zamani kwasababu zamani mtindo huu ulikuwa hupendwa kutumiwa zaidi na jinsia ya kiume tuu na pia mtindo huu asili yake ni Afrika.

Mtindo huu ni mzuri kwani hutumia nywele za asili na nitofauti na mitindo mingine ya rasta kwani mitindo hiyo mingine huhitaji uzi ama rasta za bandia kwaajili ya kusokotea na kumbuka kuwa mtindo huu wa rasta za asili huhitaji usafi wa hali ya juu pamoja na maji mengi wakati wakuzi osha.









Mitindo Ya Kusuka Nywele Kwa Watoto:

Habari wapendwa wangu, leo katika urembo ni nywele napenda kuzungumzia juu ya mitindo ya kusuka nywele kwa watoto na kwakua mitindo hii ni salama kwa afya basi inaweza kutumika kwa watoto pia. Shule nyingi za Tanzania zinataka watoto wawe na nywele ndogo au wasuke mitindo rahisi.

Mitindo hii inaweza kuwafaa watoto wako:






Chagua Mtindo Utakao Kufaa

Kama ulivyo ona kuna mitindo mingi ya kusuka nywele kwa watoto,ambapo mingine ni rahisi na inachukua muda mfupi wakati mingine ni migumu inahitaji muda mrefu na niya gharama kubwa.

Kwahiyo basi ukiwa na muda mfupi wakuji andaa unahitaji mitindo rahisi pia mtindo utakao mchagulia mtoto wako utategemea na tukio husika kwasababu mtindo wa shuleni ama safarini unaweza ukatofautiana na ule wa kwenye sherehe au shughuli nyingine ya kijamii.

Pia kumbuka mitindo ya kusuka nywele asilia ni bora na nimizuri kwa afya yako ya mwili na kwataswira yako kama mwafrika.

Friday 17 April 2015

Jinsi Ya Kubana Nywele Ndefu Za Asili

Mtindo huu wa kubana nywele ndefu za asili ni mtindo rahisi ambao unaweza bana mwenyewe nyumbani.

MAHITAJI
1.Chanuo
2.Mafuta
3.Chupio
4.Uzi

Hatua ya mwanzo chana nywele zako kwenda juu halafu funga uzi katikati ya nywele au ambapo unapendelea wewe.





 Baada yakuzifunga uzi nywele zako sasa ili kupata muonekano mzuri, chukua zile nywele za juu zinazo ning'inia alafu zifunge kijibutu hivi au ziokote kwakuzi kusanya pamoja.





Baada ya hapo chukua chupio alafu bana hapo kwenye kibutu, waweza tumia hizi chupio kubana nyuma kama nywele zinapepea na hazikubanika vizuri.


Kama ni mtoko sasa uko fresh kwakutoka.

Nywele Fupi Za Kuchana.

Nywele fupi za kuchana huu ni mtindo wa nywele ambao pia hupendwa kutumiwa na warembo wengi na pia mtindo huu ni rahisi na waharaka ambao unaweza kufanya mwenyewe nyumbani kwakuzi chana nywele zako baada yakuzipunguza kutoka saluni.

Haihitaji gharama kubwa kitana mafuta na kioo vinatosha.


Thursday 16 April 2015

Mitindo Rahisi Na Nafuu Ya Kutengeneza Nywele:

Kunyoa kipara:


Habari mpenzi, ndugu na rafiki msomaji wa blog hii, leo katika mitindo ya nywele mwanamitindo wako nimeamua kukuletea mtindo wa kunyoa kipara ambao ni mtindo rahisi na nafuu wakutengeneza nywele na hauhitaji gharama kubwa kama mitindo mingine ya nywele.

Unaweza ukasema kuwa huu sio mtindo wa nywele, lakini kiukweli ni mtindo maridadi kabisa na wanawake wengi sasa hivi wanapenda kuutumia na wanapendeza pia.

Angalia baadhi ya warembo hawa wakiwa katika mtindo wa kipara.




Kama ulivyo ona hapo warembo walivyo pendeza na mtindo huu wa kunyoa kipara pia mtindo huu mara nyingi hutumiwa zaidi na wanawake au wasichana wasio penda kufuga nywele na wengine huutumia mtindo huu kama mtindo ambao unaweza kuwafanya waonekane tofauti na wasichana
wengine kwani wasichana wengi hupenda sana nywele.